NA MWANAJUMA MMANGA

MKUU wa Wilaya ya Kati Unguja, Marina Joel Thomas, amewataka waendesha boda boda wa Wilaya hiyo kutotumia vileo wanapokua katika shughuli zao za kazi,  ili kuepusha ajali zisizokua za lazima.

Aliyasema hayo wakati akizungumza na wamiliki wa Vyombo vya usafiri barabarani bajaji na bodaboda huko katika ukumbi wa Baraza la Mji Wilaya ya Kati Dunga.

Alisema kutumia vileo kwa waendesha boda boda kunachangia ajali nyingi za barabarani, jambo ambalo linaweza kuepukika.

Aidha, aliwasisitiza kufuata taratibu za sheria zilizowekwa ikiwemo kukata leseni, Bima, leseni ya barabarani pamoja na uvaaji wa helment ili kuepusha usumbufu na mikwaruzano kati yao na askari wa barabarani.

“Niwaombe sana wamiliki wa vyombo vya boda boda na bajaji iwapo mtu atakamatwa amevunja sheria sitomuonea huruma wala muhali nitamchukulia hatua kali za kisheria iwe kunyanganya leseni ama kukizuia” alisema Mkuu huyo.