LONDON, England
BEKI wa kushoto wa Liverpool, Andy Robertson, amesaini mkataba mpya wa kuendelea kukitumikia kikosi hicho cha Merseyside hadi mwaka 2026.

Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 27, alijiunga na Liverpool mwaka 2017 akitokea Hull City kwa dau la pauni milioni nane ambapo mpaka sasa amecheza mechi 177.Robertson raia wa Scotland, anaungana na Trent Alexander-Arnold, Fabinho, Alisson na Virgil van Dijk kuongeza kandarasi mpya ya kubakia Anfield.

“Nahitaji kubakia hapa kwa muda mrefu kadiri itakavyowezekana”.Robertson ameshinda taji la Ligi Kuu England, Ligi ya Mabingwa Ulaya, Kombe la Dunia la Klabu na Uefa SuperCup.