LONDON, England
KOCHA wa Leicester City, Brendan Rodgers, amesema, licha ya mchezaji wake James Maddison kuhusishwa kujiunga na klabu mbalimbali Ulaya bado hawajapokea ofa yoyote rasmi ikikiri kuwa ni muda sasa wa kuanza kumiliki wachezaji wenye majina makubwa klabuni hapo.

Awali, Arsenal walikuwa wanahusishwa kuhitaji huduma yake kabla ya mchezaji huyo kuonekana kuwa ataendelea kubakia King Power.

“Kuna taarifa nyingi zilizomuhusu Maddison, lakini, hakukuwa na ofa yoyote rasmi mezani”, alisema, kocha huyo wa zamani wa Liverpool.

“Wachezaji kawaida yao wanahitaji kuondoka sehemu moja kwenda nyengine kukuza taaluma zao, kitu ambacho kwangu naona sawa kabisa, maana hata klabu kubwa hupoteza wachezaji pia”.Kwa sasa mchezaji huyo amejiunga na Leicester City na inaonekana atakuwepo kwa msimu wa michuano ya 2021/22 ambao tayari mechi za ligi umeshaanza.(Goal).