NA JOSEPH NGILISHO ARUSHA

ALIYEKUWA Mkuu wa Wilaya ya Hai Lengai Ole Sabaya amekana kumtambua Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro aliyemwapisha baada ya kuteuliwa kwa kuieleza Mahakama kwamba kesho yake ndo alijua kuwa aliyemwapisha alikuwa ni Mkuu wa Mkoa.

Akihojiwa na Wakili mkuu wa serikali , Tumaini Kweka, Mbele ya hakimu Mkazi Mwandamizi Odira Amworo wa mahakama ya hakimu Mkazi Arusha, katika Kesi ya unyang’anyi wa kutumia silaha na Kumpora Mali na fedha inayomkabili ,Sabaya na wenzake wawili.

Alisema siku iliyofuata ndio alitambua kuwa aliyemwapisha ni Marehemu Anne Mghwira, aliyekuwa mkuu wake wa Mkoa wa Kilimanjaro

Wakili Kweka, alimuuliza  Sabaya kwamba aliwahi kuhojiwa na Tume ya Binadamu na Utawala bora Mei 6, mwaka huu, juu ya vijana wanne aliokuwa akiwatumia ofisni kwake wakati sio waajiriwa wa umma ,Sabaya alijibu hakumbuki