NA MWANDISHI WETU

BAADA ya kukamilisha usajili kiungo mshambuliaji Pape Ousmane Sakho, ameanza mazoezi pamoja na wachezaji wenzake katika kambi inayoendelea nchini Morocco.

Licha ugeni kikosini Sakho ameonyesha kuanza kuzoeana haraka na wenzake kitu mbacho kinaonekana kitakuwa mchango mkubwa kwa timu.

Sakho 24, raia wa Senegal amejiunga moja kwa moja na kikosi kilichopo Morocco akitokea timu ya Teungueth FC ya nchini kwao.

Sakho ambaye anacheza winga wa kushoto amekuwa mchezaji muhimu wa Teungueth kwenye michuano ya Kombe la Shirikisho msimu uliopita.

Sakho anakuwa mchezaji wa nne aliyejiliwa msimu huu baada ya Peter Banda, Yusuph Mhilu na Duncan Nyoni.