LONDON, England
MENEJA wa Liverpool, Jurgen Klopp, amethibitisha kuwa klabu hiyo imefungua mazungumzo na Mo Salah juu ya mkataba mpya wa muda mrefu.

Mkataba wa sasa wa Salah, uliosainiwa mnamo 2018, umebakia chini ya miaka miwili, lakini, vyanzo vya Liverpool vina uhakika makubaliano yatafikiwa, na kwamba mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 29 atasaini baada ya Trent Alexander-Arnold, Fabinho, Alisson Becker na Virgil van Dijk.

“Ni jinsi ilivyo siku zote; hatuzungumzii juu ya vitu hivi. Najua tulibadilisha hilo kidogo na Hendo [Jordan Henderson], lakini hiyo haimaanishi kwamba kuanzia sasa tutawaambia juu ya kila hatua ndogo na mazungumzo.
“Ni kweli, ikiwa imesaliwa na miaka miwili kwenye mkataba wake unaweza kuhisi kuna