KAMPALA, UGANDA

SERIKALI nchini Uganda imezifungua barabara 76 za mjini  wakati nyengine 70 zitaendelea kufungwa mpaka zitakapokamilisha taratibu za kawaida za uendeshaji.

Waziri wa Kampala Minsa Kabanda mnamo Agosti 7 alisema amebaini kuwa kati ya barabara 178 ni 16 tu ambazo zilikaguliwa kati ya hizo 76 zilipendekezwa kufunguliwa tena wakati barabara 70 bado hazijatimiza mahitaji ya kufunguliwa.

Alisema kwamba timu za ukaguzi Jumamosi zilifunga Gazaland na barabara za ndani kwa kukataa kukaguliwa.

“Tumebaini kuwa barabara nyengine zilifunguliwa bila kutimiza matakwa ya kufuata yaliyowekwa. Tunaendelea na zoezi la utekelezaji na hatutosita kumshitaki mtu yoyote anayekiuka sheria,” Abanda alisema.

Baadhi ya masharti ya kufungua upya ni pamoja na uwepo wa maofisa wa kufuata katika milango yote ya barabara kuu,usafi wa mazingira, taa za kutosha na uingizaji hewa.