NA SABRA MAKAME, (SCCM)

MKURUGENZI Mipango ,Sera na Utafiti Ofisi ya Rais Fedha na Mipango, Saumu Khatib Haji, amewahimiza wananchi walioguswa na kampuni ya Master life Microfinance Limited, kujitokeza kwa wingi kuhakikisha wanatetea haki zao.

Aliyasema hayo wakati akizungumza na Zanzibar Leo, Mahonda Wilaya ya Kaskazini ‘A’ wakati zoezi la uhakiki likiendelea alisema amefurahishwa na zoezi hilo kwani limeenda kwa salama na amani.

Alisema uhakiki huu utafanyika kwa kila mwananchi ambae ameguswa na tatizo hilo  na kujitokeza  kufanyiwa uhakiki katika Wilaya ya Kaskazini.

“Waliojitokeza katika zoezi hilo wote ambao wameguswa kadhia hiyo  ikiwemo mzazi, mtoto na familia na ambao hawakugushwa hawakushiriki kutokana na  majukumu yao ya kawaida”alisema Saumu.

Licha ya hayo, alisema zoezi limeanza tarehe 16 mwezi huu Kaskazini ‘A’ na kumalizia tarehe saba mwezi wa tisa Pemba Wilaya ya Chake Chake eneo la kituo cha Polisi Madudu.

Mkurugenzi alisema zoezi hilo litakuwa  endelevu  na kuzishirikisha  zote za  Zanzibar, hata hivyo, anasema  litakua na muda maalumu wa kumalizika kuhakikisha wananchi wanalifanikisha hilo.

“kwanza napenda nitoe shukrani zangu za dhati kwa Wilaya ya Kaskazini, ‘A’ kuhakikisha zoezi limekwenda vizuri, hapakua na  misuko suko wala lawama za aina yoyote zilizojitokeza”alisema  Mkurugenzi.