NA FATUMA KITIMA, DAR ES SALAAM

WAZIRI wa Biashara na Maendeleo ya Viwanda wa Serikali ya Mapinduzi  ya  Zanzibar,  Omar  Said  Shaban,  amewataka wawekezaji na watoa huduma kuweka kipaumbele katika kutambua malengo ya falsafa ya Kaizen katika biashara ya uwekezaji .

Akizungumza jana jijini hapa wakati wa kufunga kongamano la siku tatu la falsafa ya Kaizen Afrika uliofanyika kwa njia ya mtandao na ana kwa ana ili kushirikishana katika ufahamu na uzoefu kuhusu matumizi endelevu ya falsafa ya kaizen wenye lengo la kuongeza ubora na tija kwenye viwanda nchi za Afrika.

Alitoa rai kwa wote ambao hawajaanza kutumia falsafa hiyo wajitahidi kutumia ili waweze kunufaika na fulsa zinazotokana na utekelezaji wake.

“Naamini matumizi ya falsafa ya kaizeni katika nyanja mbalimbali hapa nchini yamechangia katika kuiwezesha Tanzania kufikia mapema hatua ya uchumi wa kati,” alisema

Alisema Tanzania kama nchi nyingine ni Mwanachama katika mazungumzo ya kushiriki katikasoko huru la bara la Afrika, hivyo kampuni zisizokuwa na msingi imar katika ubora na uzalishaji hayawezi kushindana katika soko la Kimataifa.

Alisisitiza hali ya kuzingatia masuala ya ubora na tija watumie falsafa hiyo nchini na ameishukuru serikali ya Japan kuendelea kutoa   msaada katika nchi hizo.

Alisema matumizi ya falsafa hiyo nchini itasaidia kutatua changamoto zilizopo katika taasisi mbalimbali ikiwemo kuimarisha usalma na kuokoa muda katika maeneo yao ya kazi.

Alieleza Tanzania ni miongoni mwa nchi inayonufaika na msaada wa shirika la misaada la Japan (JAICA) katika kutekeleza programu ya kuendeleza sekta ya viwanda kwa kuimarisha ubora na tija kupitia falsafa ya kaizen.

Alifafanua kuwa ujenzi wa uchumi endelevu wa viwanda unategemea uwepo wa idadi ya kutosha ya watu wenye ujuzi na stadi zinazihitajika katika kujenga na kuendesha viwanda, sambamba na kuhudumia sekta hiyo.

Kauli mbiu ya mwaka huu ni ‘fursa ya kuongeza kasi ya maendeleo ya viwanda na biashara Afrika’ambayo imelenga kuwa moyo wadau wa biashara na viwanda kutokana na ukweli kwamba nchi za Afrika ikiwemo Tanzania imekuwa na juhudi ya kuendeleza sekta ya viwanda kuifanya kuwa sekta kiongozi katika kufikia maendeleo ya Afrika.