ZASPOTI
UONGOZI wa muda wa timu ya Shangani, umekutana kwa lengo la kujadili mambo mbali mbali ikiwemo kufanya uchaguzi mkuu wa viongozi watakaiongoza kwa miaka nne ijayo.

Shangani inayoshiriki ligi daraja la pili wilaya ya Mjini Unguja.
Akizungumza na mwandishi wa gazeti hili huko Mnazimmoja, , Mwenyekiti wa muda wa klabu hiyo, Abdulrahim Hessein, alisema, uchaguzi huo utafanyika mwanzo mwa mwezi wa tisa mwaka huu.

Alizitaja nafasi zitagombaniwa ni pamoja na mwenyekiti, katibu, wajumbe wote ikiwemo washika fedha.
Alisema mbali na kufanya uchaguzi, malengo yao ni kurejesha heshima na hadhi ya timu hiyo kama ilivyokuwa zamani.

Alisema wazee na wazawa wa Shangani wamekubali kukutana kwa lengo la kutafuta njia ya kuisaidia timu kushinda hatua zote na kufika daraja la kwanza na kuingia Ligi Kuu ya Zanzibar.
Aidha, alisema, ili kufikia malengo yao ya kuipandisha timu, wamepanga kutengeneza bajeti ili kupata fedha za kusajili wachezaji wazuri watakaofanya kazi katika timu hiyo.

Alisema katika usajili wataangalia wachezaji wazawa watakaoumizwa na timu yao kwa kila hali.
Hivyo aliwataka mashabiki wa Shangani kurudi moyo ili kushirikiana na kuisaidia timu kufikia malengo.