ADDIS ABABA, ETHIOPIA

SHIRIKA  la ndege la Ethiopia, barani Afrika, limekanusha kusafirisha silaha na wanajeshi katika eneo lenye vita la Tigray.

Wito wa kususia shirika la ndege linalomilikiwa na serikali ulionekana kwenye mitandao ya kijamii kwa madai ya kuhusika katika mzozo wa miezi tisa.

Shirika la ndege la Ethiopia linakanusha vikali madai yote yasiyo na msingi ambayo yanaendelea kwenye mitandao ya kijamii kuhusu ushiriki wa shirika hilo kusafirisha silaha za kivita na wanajeshi katika mkoa wa Tigray.

Vita vinavyogawanya vikosi vya serikali na washirika wao dhidi ya waasi wa Tigray viligharimu maelfu ya maisha na kusukuma mamia ya maelfu katika njaa, na madai ya ukiukwaji wa haki pande zote mbili.

Madai juu ya carrier huyo wa kitaifa yalionekana katika machapisho mengi ya Twitter, mengine yakifuatana na picha za wanajeshi waliopanda moja ya ndege zake.

Shirika la ndege la Ethiopia limesema ripoti hizo zilitumia picha kadhaa zilizopigwa za zamani na zisizohusiana ili kuchafua chapa ya shirika hilo.

Ndege za kwenda na kurudi Tigray, mkoa wa kaskazini mwa Ethiopia, zilisitishwa baada ya mzozo kuzuka mnamo Novemba na baada ya kufunguliwa kwa muda, anga ilifungwa tena mwezi mmoja uliopita.

Hakukuwa na ndege kuelekea eneo hilo tangu wakati huo, na hakuna ndege iliyotua katika eneo la mizozo.

Umoja wa Mataifa na mashirika mengine ya misaada yalitoa rufaa za dharura za kufunguliwa kwa njia za angani na barabara kwenda Tigray, ambapo UN inasema zaidi ya watu milioni tano wanahitaji msaada sana.