NA TIMA SALEHE, DAR ES SALAAM

KIKOSI cha timu ya Simba SC, kimeondoka jana kuelekea nchini Morocco kwa ajili ya kufanya maandalizi ya msimu ujao.

Simba SC wameondoka jana mchana baada ha wachezaji wao ambao walikuwa mapumziko na kuwasili kambini.

Maandalizi hayo ni pamoja na michuano ya kimataifa ya ligi ya mabingwa ambayo wekundu hao wa msimbazi wanatarajia kushiriki.

Akizungumza na Zanzibar Leo jana Ofisa Habari Msaidizi wa klabu hiyo Ally Shatry, alisema kwamba kikosi kimesafiri na wachezaji wote ambao walikuwa kambini.

” Timu imesafiri leo (jana) mchana kuelekea nchini Morocco wachezaji wote ambao walikuwepo kambini wamesafiri na timu,” alisema Kikosi cha Simba kimesafiri baada ya kumaliza mchakato wa kupata chanjo ya UVIKO-19.