NA ZAINAB ATUPAE

TIMU ya Soka ya Six Center imeendelea kujinyakulia pointi baada ya juzi kupata ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Nyangobo FC katika muendelezo wa mashindano ya Bahari FM ndondo cup.Mchezo huo uliotimua vumbi uwanja Blue Star majira ya saa 10:00 jioni.

Hadi mapumziko Six ilikuwa ikiongoza kwa bao moja lililofungwa na Diara Haji dakika ya 36.

Kuingia uwanjani kumalizia kabumbu hilo timu zilifanya mabadiliko kutoa na kuingiza wachezaji,lakini mabadiliko hayo yalileta mafanikio kwa Six Center  dakika 75  Wali Abdi Kombo aliongeza bao la pili.