NA HAFSA GOLO

JUMLA ya shilingi milioni 7.9 zimetumika kwa ununuzi wa photokopi ,komputa na vifaa vya ujenzi katika skuli ya msingi ya Kihinani na skuli ya Msingi Kama.

Mbunge wa jimbo la Mfenesini, Zubeida Khamis Shaib alisema viongozi wa jimbo wamedhamiria kuimarisha sekta ya elimu sambamba na kuondosha changamoto zilizopo ili kuleta ufaulu bora.

Alisema kuwepo kwa mazingira bora na rafiki kwa wanafunzi na walimu itasaidia kufikia malengo ya serikali katika  kuleta mabadiliko ya elimu na kuongezeka kwa kiwango kizuri cha ufaulu katika mitihani ya taifa.

“Fedha hizi walimu naomba zikanunuliwe umeme na dawa za huduma ya kwanza, ili wanafunzi waweze kusoma masomo ya ziada na pale watoto wanapopata tatizo la kiafya waweze kupatiwa huduma ya kwanza”,alisema.

Akizungumza na skuli ya msingi Kama, alisema lengo ni kupunguza changamoto ya idadi kubwa ya wanafunzi madarasani na waweze kujifunza vizuri.