JUBA, SUDAN KUSINI
IDARA ya polisi ya Sudan kusini imepeleka maofisa kwenye mitaa ya mji mkuu wa Juba huku ikionya wananchi dhidi ya kushiriki kwenye maandamano ya kitaifa dhidi ya serikali.
Kundi la kiraia limepanga maandamano hayo baada ya kuzindua kampeni ya kuitisha mabadiliko mwezi Julai.
Kundi hilo linadai kwamba serikali mpya ya muungano chini ya Rais Salva Kiir haijafanya chochote katika kutatua changamoto zinazowakabili watu wa Sudan Kusini.
Abraham Awlic ambaye ni mmoja ya wanachama wa kundi hilo alisema kwamba tayari waliwafahamisha poslisi kuhusu maandamano hayo kwa njia ya barua ingawa siyo lazima kufanya hivyo.
Abraham alisema watu wa Sudan kusini watajitokeza ili kuandamana ikiwa ni haki yao ya kikatiba.
Alisema kwamba huwezi kuomba idhini ya kuandamana kutoka kwa serikali inayo kandamiza.Msemaji wa polisi meja generali Daniel Justin ameonya kwamba maandamano hayo yatavuruga amani, na kamwe hatoruhusiwa na serikali.