TOKYO, JAPAN

WAZIRI Mkuu wa Japani Suga Yoshihide anasema kuimarisha mfumo wa afya ni kipaumbele ili kulinda maisha ya watu.

Alisema serikali itajenga mfumo utakaowapa mwanya wagonjwa wanaojiuguza nyumbani kufuatiliwa kwa kutembelewa au kwa kupigiwa simu na madaktari waliokutana nao mara ya kwanza hadi kituo cha afya ya umma kitakapowahudumia.

Hatua nyengine ni kupata taasisi bora za tiba katika kila eneo ili kuwahudumia wanawake wajawazito walioambukizwa virusi vya korona wakati wa dharura.

Suga pia alirejea mpango wa kuwa na taasisi zaidi za tiba za muda, kwa kuweka vifaa vya oksijeni vya kuwasaidia wagonjwa kupumua katika majengo makubwa yasiyo hospitali.