Mshamba abwagwa Jumuiya ya Wazazi

NA KHAMISIU ABDALLAH

MWENYEKITI wa Chama cha Mapinduzi Mkoa wa Mjini, Talib Ali Talib,amesisitiza suala la ushirikiano kwa viongozi wa chama katika utekelezaji wa majukumu yao, ili kukipeleka mbele chama chao na jumuiya kwa ujumla.

Aliyasema hayo wakati akifungua Mkutano Mkuu  wa wazazi Wilaya ya Amani wenye lengo la kufanya uchaguzi kumchagua Mwenyekiti wa jumuiya ya wazazi wilaya hiyo katika ukumbi wa CCM Amaani Mkoa.

Alisema ushirikiano baina ya viongozi wa jumuiya na wanachama ndio silaha muhimu katika kuivusha jumuiya yao na chama kwani ndio jumuiya pekee yenye heshima kubwa ambayo imeleta uhuru ndani ya Tanzania.

“Kama kiongozi ukikaa basi utambue jumuiya ya wazazi ndio jumuiya pekee yenye namaadili ndani ya CCM na Tanzania kutokana na heshima yake kubwa iliyokuwa nayo kiongozi anatakiwa jumuiya hiyo aiheshimu kwa kufuata kanuni na maadili ya chama,” alisema.

Akizungumzia kuundwa kwa jumuiya hiyo, alisema imeundwa kwa makusudi ili kuhakikisha watu wanapata elimu na kuwa viongozi bora watakaoongoza nchi yao ya Tanzania.