KABUL, Afghanistan

WATU wasiopungua watatu wameuawa na wengine zaidi ya kumi wamejeruhiwa katika maandamano ya kupinga Wataliban kwenye mji wa Jalalabad ulio magharibi mwa Afghanistan.

Walioshuhudia tukio hilo walisema wanamgambo hao wa itikadi kali ya kiislamu waliwashambulia kwa bunduki watu ambao walikuwa wakipandisha bendera ya Afghanistan katika uwanja wa mmoja wa mjini humo.

Wakati huo huo Umoja wa Ulaya, Marekani, Uingereza na nchi kadhaa nyengine zimetaka haki za binadamu ziheshimiwe nchini Afghanistan.

Katika tangazo lao la pamoja, nchi hizo zilisema wanawake na wasichana wanayo haki ya kuishi salama na kwa uhuru kama raia wengine wa Afghanistan.

Huko mjini Kabul, viongozi wa Taliban walifanya mazungumzo na rais wa zamani wa Afghanistan Hamid Karzai pamoja na aliyekuwa ofisa mwandamizi katika utawala ulioangushwa, Abdullah Abdullah, mada kuu ikiwa namna ya kuunda serikali.