ZASPOTI

NYOTA wa Bafana Bafana, Percy Tau amejiunga na Al Ahly kwa mkataba wa mkopo baada ya kukubali mpango wa kuihama klabu ya Brighton & Hove Albion ya England.
Na kilichobakia ni Tau kufuzu vipimo vya afya na kumwaga wino rasmi kuwa mchezaji wa Al Ahly.

Kurejea kwa Percy Tau barani Afrika kumegawanya maoni ya mashabiki wa soka nchini humo na wengine wakiamini kwamba atakuwa akifanya uamuzi mbaya wa soka yake.
Lakini, matamanio ya Pitso Mosimane kuendelea kutawala soka ya Afrika na kushinda Kombe la Dunia la Klabu la FIFA na Al Ahly ilikuwa dhahiri vya kutosha kumshawishi Tau kurejea ‘nyumbani’.

Tau na Mosimane walifanya kazi pamoja kwa miaka kadhaa Mamelodi Sundowns kabla ya mchezaji huyo anayetumia mguu wa kushoto kujiunga na Brighton mnamo 2018.
Tau alitumia misimu kadhaa kwa mkopo nchini Ubelgiji wakati akijitahidi kupata kibali cha kufanya kazi nchini Uingereza hadi mapema 2021 wakati Brighton alipomkumbuka.(Goal).