NA VICTORIA GODFREY

TIMU zinazoshiriki ligi daraja la Tatu wilaya ya Kigamboni zimetakiwa kuzingatia nidhamu katika michezo yao.

Rai hiyo imetolewa na Mjumbe wa Kamati ya Mashindano ya Chama cha Mpira wa Miguu Wilaya ya Kigamboni ( KDFA) Swedi Hamis, ambapo alisema timu ambayo itaonyesha utovu wa nidhamu itachukuliwa hatua inayostahili.

Alisema tayari wameweka mazingira mazuri kwa kuendesha semina elekezi kwa klabu na wadau, ili kupeana mwongozo wa ligi na kuepuka malalamiko .

“Tunaomba mashabiki kujitokeza kwa wingi ila wazingatie nidhamu uwanjani,atakayekiuka hatusita kumchukulia hatua,kwani tunahitaji kuona ligi yetu inakuwa bora na ushindani,” alisema Hamis.