PAUL POGBA
PARIS ST-GERMAIN itatoa ofa kwa kiungo wa kati wa Manchester United raia wa Ufaransa, 28, Paul Pogba na makubaliano yenye thamani ya pauni 510,000 kwa wiki kama hatua ya kujaribu kumsajili nyota huyo aliyewahi kushinda Kombe la Dunia kupitia uhamisho wa bure msimu ujao. (Independent)
HARRY KANE
MANCHESTER CITY kuendelea na juhudi za kumsajili mshambuliaji wa England Harry Kane kutoka Tottenham, licha ya Spurs kusema mara kadhaa kwamba haiko tayari kumuuza mchezaji huyo, 28. (ESPN)
JUDE BELLINGHAM
CHELSEA inataka kumnunua mchezaji wa Borussia Dortmund Jude Bellingham, 18, kama mbadala wa mchezaji mwenzake wa timu ya England Declan Rice, 22. (Eurosport, via Sun)
JORDAN HENDERSON
MCHEZAJI wa Liverpool kiungo wa England Jordan Henderson, 31, amefikia makubaliano ya mkataba mpya wa muda mrefu na klabu hiyo. (The Athletic – subscription required)
JOAN LAPORTA
RAIS wa Barcelona Joan Laporta amesema kuwa kushindwa kwa watangulizi wake kuwekeza tena pauni milioni 200 kutoka kwa MBrazil Neymar mwaka 2017 wakati anajiunga na PSG kumechangia mgogoro wa kifedha unaokumba klabu. (Times)
CRISTIANO RONALDO
MANCHESTER UNITED wamearifiwa juu ya mpango ambao huenda unaendelea kwamba Juventus na Cristiano Ronaldo, 36, wanasemekana wanashughulikia mpango wa kuondoka kwa mshambuliaji huyo wa Ureno. (La Repubblica – in Italian)
MARTIN ODEGAARD
MCHEZAJI wa Real Madrid Martin Odegaard, 22, huenda anakaribia kurejea Arsenal, baada ya wakala wake raia wa Norway kwenda London kufanya mazungumzo ya makubaliano ya mkopo wa muda mrefu. (Mirror)
AMAD DIALLO
Winga wa Manchester United raia wa Ivory Coast Amad Diallo, 19, anahitajika kwa mkopo na klabu ya Sheffield United. (talkSPORT)
HARVEY BARNES
WINGA wa Leicester City, 23, Harvey Barnes yuko tayari kusaini mkataba mpya na wanaoshikilia kombe la FA. (The Athletic, subscription required)
PIERRE-EMERICK AUBAMEYANG
ARSENAL huenda ikakubali kumuuza Pierre-Emerick Aubameyang kwa sabau mchezaji huyo, 31, mshambuliaji raia wa Gabon hawana maelewano mazuri na kocha wa Gunners Mikel Arteta. (talkSPORT)
GRANIT XHAKA
KIUNGO wa kati wa Arsenal Granit Xhaka, ambaye alikuwa anajadiliwa huko Roma mapema msimu huu amesaini mkataba mpya na Gunners. (Guardian)
KYLE HUDLIN
MANCHESTER CITY ni miongoni mwa klabu zinavyomnyatia mchezaji mrefu zaidi wa Uingereza, futi 6 na nchi 9 wa Solihull Moors mshambuliaji Kyle Hudlin, 21. Middlesbrough na Cardiff City pia nazo zilikuwa zinamfuatilia. (The Athletic, subscription required)
EMERSON PALMIERI
CHELSEA inafanya mazungumzo na Lyon juu ya uhamisho wa beki wao wa kushoto raia wa Italia Emerson Palmieri, 27, wakati kocha wa Blues Thomas Tuchel anaangalia namna ya kupunguza kikosi chake. (Guardian)