Boubacar Kamara
NEWCASTLE United wanaangalia uwezekano wa kuingia mkataba na kiungo wa Mfaransa, Boubacar Kamara (21), kutoka Marseille kwa takriban pauni milioni 10. (Mail).

Romelu Lukaku
CHELSEA haijakata tamaa ya kusaini tena mkataba na mshambuliaji wa Ubelgiji, Romelu Lukaku (28), kutoka klabu ya ‘Serie A’ ya Inter Milan. (Athletic).

Harry Kane
MANCHESTER City wamepungukiwa na pauni milioni 40 kati ya pauni milioni 160 bei ambayo Tottenham inataka kumuuza mshambuliaji wa England, Harry Kane (27). (Star).

Lionel Messi
BARCELONA wapo tayari kutangaza rasmi mkataba mpya wa miaka mitano wa mshambuliaji Muargentina, Lionel Messi (34), katika siku zijazo. (Sport).

Aaron Ramsey
KLABU ya Newcastle United imeuliza juu ya uwezekano wa kumsajili kiungo wa kati wa Juventus raia wa Wales, Aaron Ramsey (30). (Goal).

Erling Braut Haaland
MANCHESTER United ina miezi 12 ya kumshawishi mshambuliaji wa Borussia Dortmund raia wa Norway, Erling Braut Haaland kwamba ni klabu sahihi kwake. Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 21 ambaye anasakwa na Chelsea anatarajiwa kuhama katika msimu wa kiangazi wa mwaka 2022. (Manchester Evening News).

James Ward-Prowse
ASTON Villa imewasilisha ofa ya pili kwa ajili ya kiungo wa Southampton (26), Muingereza James Ward-Prowse baada ya ofa ya awali ya pauni milioni 25 kukataliwa. (Mail).

Marco Asensio
KLABU za Leicester City, Leeds United na Everton zinashindana kumsaini winga wa Real Madrid Muhispania, Marco Asensio (25). (Fichajes).

Kieran Trippier
KLABU ya Atletico Madrid wanajiandaa kumuuza mlinzi, Kieran Trippier (30), kwa klabu ya Manchester United ili kujiandaa kumchukua mchezaji wa Roma, Alessandro Florenzi (30), kama mbadala wa mchezaji huyo wa kimataifa wa England. (AS).

Ronaldo Vieira
KLABU ya Sheffield United ipo katika mazungumzo kwa ajili ya kuingia mkataba na kiungo wa kikosi cha zamani cha England chini ya umri wa miaka 21, Ronaldo Vieira (23), kutoka Sampdoria. (Mail).

Jose Mourinho
MENEJA wa Roma, Jose Mourinho yuko makini kumsajili mchezaji wa Borussia Dortmund, Mdenmark Thomas Delaney (29), baada ya kushindwa kusaini mkataba na mchezaji wa kimataifa wa Uswisi, Granit Xhaka (28), kutoka Arsenal. (Sun).

Conor Coady
KLABU ya Tottenham ipo katika mazungumzo ya awali na Wolves kuhusu kusaini mkataba na Conor Coady huku meneja wa Spurs ,Nuno Espirito Santo akiwa makini kujumuika tena na mlinzi huyo Kaskazini mwa London. (Football Insider).

Simone Inzaghi
MENEJA wa Inter Milan Simone Inzaghi ameazimia kuendelea kumsaka kiungo wa safu ya nyuma-kushoto wa Chelsea Marcos Alonso,30. (Calciomercato – in Italian)

Matthew Hoppe
KLABU ya Arsenal na Everton wamekuwa wakihusishwa na uhamisho wa mshambuliaji wa klabu ya Schalke, Mmarekani Matthew Hoppe (20). (Star).

Willy Caballero
MLINDA mlango wa Argentina, Willy Caballero anahusishwa na kurejea katika Ligi ya Hispania ya Malaga baada ya kuachiwa na Chelsea msimu huu. (Marca).

Philip Billing
KLABU ya Norwich City imeanza mazungumzo na Bournemouth juu ya kusaini mkataba na kiungo raia wa Denmark Philip Billing (25). (Football Insider).