Yoane Wissa
KLABU ya Brentford wanakamilisha kusaini mkataba na winga wa Congo, Yoane Wissa mwenye umri wa miaka 24 kutoka klabu ya Ufaransa ya Lorient. (Sky Sports).

Lionel Messi
TANGAZO la Barcelona kwamba mshambuliaji wa Argentina, Lionel Messi (34), hatabakia kwenye klabu hiyo ‘limefungua mlango wa uhamisho wa kushtua huko Manchester City. (Manchester Evening News).

KUWEPO kwa Messi kunaweza kuathiri uwezekano wowote wa uhamisho ambao ManCity walikuwa wanaupanga kwa ajili ya mshambuliaji wa Tottenham na England, Harry Kane (27). (Express).

Romelu Lukaku
PENDEKEZO la Romelu Lukaku la kuhamia tena Chelsea huenda likawa linakaribia kukwama kwani mwenyekiti wa klabu ya Inter Milan, Steven Zhang anataka kufikiria kwa muda zaidi kabla ya kuamua iwapo anataka kumuuza mshambuliaji huyo Mbelgiji mwenye umri wa miaka 28. (Gazzetta dello Sport).

Kieran Trippier
MANCHESTER United bado wapo makini na kusaini mkataba na mlinzi wa England, Kieran Trippier, lakini Atletico Madrid wanakataa kupunguza bei yao ya pauni milioni 34 ili kumtoa mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 30. (Sun).

Joaquin Correa
ARSENAL wamefanya ofa ya takriban dola milioni 17 kwa ajili ya mshambuliaji wa Lazio, Muargentina Joaquin Correa (26), ambayo inaangaliwa kuwa haitoshi na klabu hiyo ya Roma. (Corriere dello Sport).