ZASPOTI

Takefusa Kubo
WINGA wa Real Madrid na Japan, Takefusa Kubo, anakaribia mkopo wa pili kwenda Mallorca baada ya miamba hiyo ya Balearic kuwapiga bao wapinzani wake, Real Sociedad kwa huduma yake.

Yoso huyo mwenye umri wa miaka 20 alitua ‘La Liga’ kuelekea kampeni ya 2019-20, na ametumia misimu yake miwili ya kwanza huko Hispania mahali pengine kwa muda mfupi kwa amri ya Los Blancos.(Goal).

Kylian Mbappe
KLABU ya Paris Saint-Germain itampa Kylian Mbappe mkataba wa mshahara ulioongezwa ili kumshawishi abakie klabuni hapo.
Mchezaji huyo wa kimataifa wa Ufaransa amehamasishwa na kuondoka Parc des Princes msimu huu wa joto baada ya msimu mbaya kwa klabu na nchi yake.(Le10Sport).

Renato Sanches
BARCELONA wamekubaliana na kiungo wa Ureno, Renato Sanches (23), lakini, hawajakubaliana ada na klabu yake ya Lille. (Le10 Sport).

Nikola Milenkovic
WEST Ham United wamesalia kwenye mazungumzo na Fiorentina kuhuhu dili la pauni milioni 14 kwa ajili ya mlinzi, Nikola Milenkovic (23), lakini watakabiliwa na ushindani kutoka Juventus. (Mail).

Duje Caleta-Car
KLABU ya West Ham United pia inamtaka mlinzi wa Marseille, Duje Caleta-Car (24), baada ya mlinzi huyo wa kati kukataa ofa msimu wa joto uliopita.( L’Equipe).

Josh Sargent
MSHAMBULIAJI raia wa Marekani, Josh Sargent (21), anakaribia kumaliza hatua za uhamisho kuhamia Norwich City akitokea Werder Bremen. (Goal).

Martin Odegaard
REAL Madrid wamezuia uhamisho wa kiungo wa Norway, Martin Odegaard (22), kwenda Arsenal baada ya Toni Kroos kupata maumivu. (AS).

James Ward-Prowse
KLABU ya Southampton imekataa dau la pauni milioni 25 kutoka kwa Aston Villa kwa ajili ya James Ward-Prowse (26), na haina nia ya kumuuza kiungo huyo msimu huu.( Football Insider).

Matthijs de Ligt
CHELSEA inamtaka mlinzi wa Juventus, Matthijs de Ligt (21), inaweza kutoa ofa ya pauni milioni 50 na mshambuliaji, Timo Werner (25). Hata hivyo Juve inamtaka zaidi kiungo wa kati Muitaliano, Jorginho (29), sambamba na kitita cha fedha. (Calciomercatoweb).

Nayef Aguerd
WEST Ham wametangaza dau la pauni milioni 15 kwa ajili ya mlinzi anayekipiga Rennes Nayef Aguerd (25), klabu hiyo ya Ufaransa ikitarajiwa kukataa ofa hiyo. (Football Insider).