ZASPOTI

Freddie Woodman
MENEJA wa Arsenal, Mikel Arteta, huenda akamgeukia kipa wa Newcastle United, Muingereza Freddie Woodman (24), baada ya kushindwa kumsaini kipa wa Sheffield United na England, Aaron Ramsdale (23). (Chronicle).

Pau Torres
KLABU ya Tottenham ipo tayari kumnunua beki wa Villarreal na Hispania, Pau Torres (24), ambaye bei yake inakadiriwa kuwa pauni milioni 55 pia ananyatiwa Manchester City, Liverpool na Manchester United. (Times).

Adama Traore
LIVERPOOL bado wanataka kumsaini winga wa Wolves na Hispania, Adama Traore (25), kabla dirisha la uhamisho kufungwa. (90min).

Martin Odegaard
REAL Madrid wanajiandaa kumuuza kiungo wa Norway, Martin Odegaard msimu huu wa joto. Arsenal ipo tayari kuwasilisha dau la kumnunua kiungo huyo mwenye umri wa miaka 22 ambaye alipata ufanisi mkubwa katika mkataba wake wa bure na washika bunduki msimu uliopita. (Goal).

Ben Davies
MLINZI wa Liverpool, Ben Davies yuko mbioni kufanya mkopo wa msimu mzima kwenda Sheffield United.
Beki huyo wa kati anaelekea Yorkshire, ambapo atakuwa sehemu ya safu ya ulinzi ya kocha mpya, Slavisa Jokanovic.(Sky Sports News).

KLABU ya West Ham inafuatilia uhamisho wa beki wa Aston Villa, Kortney Hause.
Mchezaji huyo wa zamani wa vijana wa England ambaye mwanzoni aliwasili Villa Park kutoka Wolves mnamo 2019, ameona nafasi zake zikiwa zimezuiliwa katika misimu michache iliyopita. (Football Insider).

Kalidou Koulibaly
KLABU ya Paris Saint Germain inaweza kumchukua beki wa Napoli, Kalidou Koulibaly.
Miamba hiyo ya ‘Ligue 1’ inatafuta beki wa kujaza nafasi wakati Sergio Ramos ameumia, na nyota huyo wa Senegal anaweza kuwa chaguo bora, akiwa ni ghali.(Gazzetta dello Sport).

Houssem Aouar
ARSENAL itatoa ofa ya mkopo kwa nyota wa Lyon, Houssem Aouar ikiwa hatua zao nyengine zilizopangwa zitafaulu.
Washika bunduki wanatafuta kumuongeza Martin Odegaard au James Maddison kwenye kiungo majira haya ya joto juu ya makubaliano ya kudumu.(The Sun).

Michy Batshuayi
MSHAMBULIAJI wa Chelsea, Michy Batshuayi anakaribia kuhamia Besiktas.
Batshuayi hajaonekana kuwa katika mipango ya ‘Blues’ ya 2021-22, na kuwasili kwa Romelu Lukaku hivi karibuni kunamshinikiza zaidi kwenye chati ya kina kirefu. (Goal).

Jordan Henderson
KOCHA, Jurgen Klopp amesisitiza Liverpool itaamua mustakabali wa Jordan Henderson, wakati mazungumzo juu ya mkataba mpya wa nahodha huyo wa Liverpool yanaendelea.
Henderson ameingia miaka miwili ya mwisho ya makubaliano yake ya sasa huko Anfield. (Goal).