Marco Asensio
KLABU ya Arsenal huenda iko tayari kwa makubaliano ya mabadilishano yatakayogharimu kiasi cha pauni milioni 34 kumpata mchezaji wa Real Madrid raia wa Hispania, Marco Asensio (25). (Fichajes).

Nikola Milenkovic
KLABU ya Tottenham imeimarisha nia yake ya kumsaka mlinzi wa Fiorentina raia wa Serbia, Nikola Milenkovic baada ya West Ham kuamua kutomfuatilia mchezaji huyo. (The Times).

Mohamed Salah
MSHAMBULIAJI wa Misri, Mohamed Salah (29), huenda akafikia mkataba wa muda mrefu na Liverpool. (Times).

Harry Kane
MANCHESTER City ipo tayari kulipa pauni milioni 150 kumsajili mshambuliaji wa England, Harry Kane (28), kutoka Tottenham.
Kane ana matumaini kuwa hatma yake itakuwa wazi zaidi wiki ijayo baada ya Spurs kuanza kampeni yao ya ligi kuu nyumbani dhidi ya ManCity. (Telegraph).

Cristiano Ronaldo
KLABU ya Paris St-Germain itatafuta saini ya mshambuliaji wa Ureno, Cristiano Ronaldo (36), kutoka Juventus msimu wa joto wa 2022 kama mbadala wa mshambuliaji wa Ufaransa mwenye umri wa miaka 22, Kylian Mbappe, ambaye amekuwa mlengwa wa muda mrefu wa Real Madrid. (AS).

Philippe Coutinho
KIUNGO wa Brazil, Philippe Coutinho anahusishwa na kurejea Liverpool akitokea Barcelona, klabu aliyoondoka Merseyside kujiunga nacho kwa pauni milioni 142 mnamo Januari 2018. Everton, Manchester United, Chelsea, Arsenal, Tottenham na Leicester City hivi karibuni zimehusishwa na nyota huyo mwenye umri wa miaka 29. (Liverpool Echo).

Jeremy Doku
LIVERPOOL inasemekana pia inavutiwa na mshambuliaji wa Ubelgiji, Jeremy Doku kutoka Rennes, ambayo itahitaji pauni milioni 38 kwa mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 19. (Voetbal24).

Antonio Rudiger
KLABU za Real Madrid na Paris St-Germain zinafuatilia hali ya beki wa kati wa Ujerumani, Antonio Rudiger huko Chelsea, wakijua kwamba makubaliano ya mkataba wa mapema yanaweza kusainiwa na mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 28 mnamo Januari. (Sky Sport).

Pau Torres
KLABU ya Tottenham inaweza kumchukua beki wa Villarreal mwenye umri wa miaka 24, Pau Torres. (Express).

Lewis O’Brien
KLABU ya Crystal Palace inajiandaa kushindana na Leeds United katika harakati za kumfuata kiungo wa Huddersfield Town mwenye umri wa miaka 22, Lewis O’Brien.(Football Insider).

James Ward-Prowse
KOCHA wa Southampton, Ralph Hasenhuttl, ameazimia kumbakisha kiungo wa England mwenye umri wa miaka 26, James Ward-Prowse ambaye anatafutwa na Aston Villa na Tottenham. (Football London).

Amad Diallo
MANCHESTER United iko tayari kumruhusu mshambuliaji wa Ivory Coast mwenye umri wa miaka 19, Amad Diallo aondoke kwa mkopo msimu huu wa joto. (Manchester Evening News).

Nayef Aguerd
KLABU ya West Ham imepata pigo baada ya ofa yao ya pauni milioni 17 kwa beki wa Morocco mwenye umri wa miaka 25, Nayef Aguerd kukataliwa na Rennes. (Football Insider).

Kent Ryan
KLABU ya Leeds United inaweza kufanya juhudi mpya kumsaini mshambuliaji wa Uingereza mwenye umri wa miaka 24, Kent Ryan kutoka Ranger baada ya kampeni ya klabu hiyo ya Scotland ya Ligi ya Mabingwa kumalizika. (Athletic).

Mikel Arteta
MENEJA wa Arsenal Mikel Arteta bado ana matumaini ya usajili zaidi kabla ya tarehe ya mwisho ya uhamisho. (ESPN).

Diego Costa
MSHAMBULIAJI wa Hispania, Diego Costa (32), yuko mbioni kuanza tena taaluma yake huko Brazil na Atletico Mineiro, kwani hajacheza tangu alipoondoka Atletico Madrid mnamo Disemba. (Goal).

Neto
MLINDA mlango wa Barcelona mwenye umri wa miaka 32, Neto anaweza kuhamia Arsenal katika msimu huu wa joto, lakini, uhamisho wa mkopo pia unawezekana .(Athletic).