Ismaila Sarr
KLABU ya Watford haijapata ofa yeyote anayemwinda winga wa Senegal, Ismaila Sarr (23), msimu huu na amesalia kuwa mchezaji imara ambaye amehusishwa na kuhamia Liverpool, lakini hauzwi. (Watford Observer).

Jesse Lingard
KIUNGO wa England, Jesse Lingard (28), yuko tayari kuondoka Manchester United kabla ya dirisha la uhamisho kufungwa pengine tu iwe anaamini atacheza mara kwa mara kwenye timu ya Ole Gunnar Solskjaer msimu huu. (Times).

Robert Lewandowski
MSHAMBULIAJI wa Poland, Robert Lewandowski yuko tayari kwa changamoto mpya mbali na Bayern Munich. Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 32, bado amesalia na miaka miwili kumaliza mkataba wake na mabingwa hao wa Bundesliga. (Mirror).

Aurelien Tchouameni
CHELSEA imeripotiwa kufanya mazungumzo mapya na kiungo wa Monaco, Aurelien Tchouameni. Mfaransa huyo mwenye umri wa miaka 21 pia amehusishwa na Manchester United katika chote cha msimu. (Simon Phillips).

Mohamed Salah
Liverpool wanaandaa ofa mpya ya mkataba kwa mshambuliaji wa Misri, Mohamed Salah, 29, ambayo itakuwa ghali zaidi katika historia ya kilabu. (Athletic – subscription required)

Pierre-Emerick Aubameyang
MSHAMBULIAJI, Pierre-Emerick Aubameyang anafurahia kusalia Arsenal hata baada ya kipindi cha uhamisho. Barcelona ilisemekana kuwa na nia ya kumsajili mshambuliaji huyo wa Gabon lakini mchezaji huyo wa miaka 32 anataka kutimiza lengo lake la kuwa gwiji wa Gunners. (Express).

Darwin Nunez
KLABU ya Brighton ipo kwenye mazungumzo na Benfica juu ya uhamisho wa pauni milioni 25 kwa mshambuliaji wa Uruguay Darwin Nunez (22). (Mail).

Amad Diallo
KLABU ya Sheffield United inavutiwa kumsajili winga wa Manchester United na Ivory Coast, Amad Diallo (19), kwa mkopo. (Sky Sports).

Isaac Success
SHEFFIELD United imeripotiwa kumruhusu mmoja wa wachezaji wao aondoke wakati ambapo mshambuliaji wa Nigeria, Isaac Success (25), anapaswa kufanya uchunguzi wa matibabu na Udinese ya Italia. (Gianluca di Marzio).

Dusan Vlahovic
RAIS wa Fiorentina, Rocco Commisso, amesisitiza kuwa hajaweka bei ya kumuulizia mlengwa wake anayechezea Manchester City na Tottenham, Dusan Vlahovic. Mshambuliaji huyo wa Serbia mwenye umri wa miaka 21 tayari amevutia dau la euro milioni 70 kutoka kwa mabingwa wa Hispania, Atletico Madrid. (TGR Rai Toscana).

Kylian Mbappe
KOCHA wa Paris St-Germain, Mauricio Pochettino, amesema, mshambuliaji wa Ufaransa Kylian Mbappe (22), ni mtulivu tu licha ya uvumi mpya unaomuhusisha na kuhamia Real Madrid. (Metro).

Thierry Small
KLABU ya Southampton inafikiria kumchukua beki wa Everton, Thierry Small. Kijana huyo mwenye umri wa miaka 17 amehusishwa na kuondoka Goodison Park wakati kuna ripoti kwamba amekataa kutia saini mkataba mpya na Toffees. (Hampshire Live).

Ilaix Moriba
BARCELONA inataka pauni milioni 12.8 kwa kiungo wa Hispania, Ilaix Moriba. Kijana huyo ananyatiwa na Wolves, lakini, klabu hiyo ya Katalunya bado hakijapokea ofa inayokubalika. (ARA via Molineux News).

Samuel Umtiti
KLABU ya Everton imewasiliana na Barcelona kumchunguza beki wa kati, Samuel Umtiti (27), kwa nia ya kutaka kumsajili mchezaji huyo wa kimataifa wa Ufaransa kabla ya tarehe ya mwisho ya uhamisho mnamo Agosti 31. (Express).