Pierre-Emerick Aubameyang
KLABU ya Arsenal ipo tayari kusikikiza ofa kwa ajili ya nahodha wake, Pierre-Emerick Aubameyang (32), na hawatamzuia iwapo mshambuliaji huyo wa Gabon iwapo atataka kuondoka kabla ya kufungwa kwa dirisha la usajili. (Telegraph).

Mikel Arteta
ARSENAL pia wamedhamiria kumuunga mkono kocha wa timu hiyo aliyeko kwenye shinikizo kubwa, Mikel Arteta kufuatia vipigo viwili ilivyovipata kwenye Ligi Kuu England. (Mirror).

Harry Kane
MWENYEKITI wa Tottenham, Daniel Levy, hatapunguza thamani ya mshambuliaji wa England, Harry Kane (28) na yuko tayari hata kukataa ofa kubwa ya kuvunja rekodi ya uhamisho Uingereza inayokaribia pauni milioni 150 kutoka Manchester City. (Telegraph).

Saul Niguez
CHELSEA wanafikiria kumchukua kwa mkopo kiungo wa Atletico Madrid na Hispania, Saul Niguez (26), wakati huo huo ‘The Blues’ imewapa mikataba mipya walinzi wake, Antonio Rudiger (28), raia wa Ujerumani na Mdenmark Andreas Christensen (25). (Telegraph).

Declain Rice
KIUNGO wa England, Declan Rice (22) amepanga kukataa ofa yoyote ya kusaini mkataba mpya kutoka klabu yake ya West Ham kama mgomo baada ya kuwekewa bei ya juu na kufanya ugumu wa yeye kuhama msimu huu.(Goal).

Jules Kounde
CHELSEA ina matumaini ya kumsajili mlinzi wa Kifaransa, Jules Kounde kutoka Sevilla huku kukielezwa kwenye mkataba wake kuna kipengele cha pauni milioni 77 ili kumruhusu kinda huyo mwenye umri wa miaka 22 kuhama. Klabu hizo mbili zilitumai beki wa Chelsea, Kurt Zouma (26), angejumuishwa kwenye mpango huo, lakini aligoma kujiunga na klabu hiyo ya La Liga. (90Min).

Eduardo Camavinga
MANCHESTER United bado inamtaka kiungo wa Rennes, Eduardo Camavinga (18), lakini, inaona nyota huyo wa kimataifa wa Ufaransa angetamani kujiunga na Paris St-Germain au klabu ya Hispania. (ESPN).

Jonathan Bamba
WEST Ham inaangalia kama wanaweza kumsajili kiungo Mfaransa wa Lille, Jonathan Bamba (25), kama mbadala wa kiungo wa kimataifa wa England, Jesse Lingard kutoka Manchester United. (Express).

Eddie Nketiah
KLABU ya Crystal Palace inajiandaa kutoa kitita cha pauni milioni 10 kwa ajili ya mshambuliaji wa Arsenal, Eddie Nketiah (22), lakini, washika bunduki hao wanataka dau la angalau linalokaribia pauni milioni 20. Nyota huyo anayeshikilia rekodi ya mabao kwenye timu ya taifa ya England chini ya miaka 21 pia amekuwa akiwaniwa na klabu za Ujerumani. (Athletic).

Lucas Torreira
KIUNGO wa Arsenal, Lucas Torreira (25), anakaribia kutua Fiorentina kwa mkopo baada ya kuisaidia Atletico Madrid, chini ya Diego Simeone kushinda taji la ‘La Liga’ msimu uliopita alikokua anacheza kwa mkopo. (football.london).

Willian
KIUNGO wa Brazil, Willian (33), yuko njiani kuondoka Arsenal bure na kujiunga na Corinthians ya nyumbani kwao, mazungumzo yako katika hatua za mwisho. (Mail).

Kieffer Moore
KLABU ya Wolves ipo tayari kutoa ofa ya pauni milioni 7 kwa ajili ya mshambuliaji wa Cardiff City na Wales, Kieffer Moore (29). (Football Insider).

Phil Jones
BEKI wa Manchester United, Phil Jones yuko tayari kwenda kwa mkopo kwenye klabu ya Championship, kwa sasa beki huyo Muingereza mwenye umri wa miaka 29 hana uhakika wa namba Old Trafford. (Football League World).

Maxwel Cornet
KLABU za Newcastle United na West Ham vitapigana vikumbo kupata saini ya mlinzi wa kushoto wa Burnley raia wa Ivory Coast, Maxwel Cornet (24), kutoka Lyon. (90 Min).