Kurt Zouma
KLABU ya West Ham pia wana matumaini ya kumsajili mlinzi wa kati wa Ufaransa, Kurt Zouma kutoka Chelsea baada ya jaribio la kumsajili mlinzi huyo mwenye miaka 26 kwenda vyema. (Telegraph).

Kylian Mbappe
REAL Madrid imepeleka ofa ya kwanza ya pauni milioni 137 kwa ajili ya mshambuliaji wa Paris St-Germain, Kylian Mbappe (22), lakini, klabu hiyo ya Ufaransa inatarajia kukataa ofa yoyote kwa ajili ya nyota huyo aliyebakisha mkataba wa mwaka mmoja. (Mail).

Richarlison
KLABU ya Paris Saint Germain inaweza kumuwania mshambuliaji wa Everton na Brazil, Richarlison (24), kama mbadala wa Mbappe. (Eurosport).

Cristiano Ronaldo
MSHAMBULIAJI wa Juventus na Ureno, Cristiano Ronaldo (36), atashawishi ahamie kwa mabingwa wa Ligi Kuu ya England, Manchester City katika wiki hii ya mwisho la usajili, huku nyota huyo wa zamani wa Manchester United angetamani kutohitimisha mkataba wake wa mwaka mmoja uliosaliama Waitaliano hao. (L’Equipe).

Bernardo Silva
RONALDO amezungumza kuhusu uhamisho huo na nyota wenzake wa Ureno, Bernardo Silva, Ruben Dias (24), na mlinzi Joao Cancelo (27). Kiungo mshambuliaji Silva au beki wa ManCity Mhispania, Aymeric Laporte, wote wakiwa na miaka 27, wanaweza kujumuishwa kwenye mpango huo wa kubadilishana wachezaji. ManCity ipo tayari kulipa mshahara atakaohitaji Ronaldo, lakini, hawako tayari kulipa kitita kikubwa cha ada ya uhamisho wake. (L’Equipe).

Erling Braut Haaland
MANCHESTER United ipo katika nafasi nzuri ya kumsajili mshambuliaji wa Borussia Dortmund na Norway, Erling Braut Haaland msimu ujao. Kinda huyo mwenye miaka 21 amekuwa lulu sokoni baada ya kufunga magoli 62 katika mechi 63 alizowachezea Wajerumani hao wa Ligi ya Bundesliga. (Bild).

Saul Niguez
CHELSEA huenda ikakabiliana na Manchester United kama watajitosa kujaribu kunasa saini ya kiungo wa Atletico Madrid na Hipsania, Saul Niguez (26), kwa mkopo. (Guardian).

Pablo Sarabia
KAMA Saul ataondoka Atletico Madrid imemuorodhesha kiungo wa Hispania, Pablo Sarabia kutoka Paris St-Germain kama mbadala wake. (Marca).

Kieran Trippier
ARSENAL imefanya mazungumzo na Atletico Madrid kuhusu uhamisho wa beki wa kulia wa England, Kieran Trippier, ingawa beki huyo mwenye miaka 30 angetamani kwenda Manchester United kama atatakiwa kuondoka Madrid. (Goal).

Willian
WINGA wa Brazil, Willian (33), beki wa kulia wa England, Ainsley Maitland-Niles (23), mshambuliaji wa Kiingereza Eddie Nketiah (22), mlinzi wa Hispania, Hector Bellerin (26), kiungo wa Uruguay, Lucas Torreira (25), winga Muingereza Reiss Nelson (21), na beki wa kushoto wa Bosnia, Sead Kolasinac (28) huenda wakatupiwa virago Arsenal wiki ijayo. (Standard).

Gaetan Laborde
WEST Ham wanapanga kupeleka ofa kwa ajili ya mshambuliaji wa Montpellier, Gaetan Laborde (27), lakini, timu hiyo ya ‘Ligue 1’ inaweza kuhitaji angalau pauni milioni 12.5 kwa ajili ya Mfaransa huyo. (Le 10 Sport).

Nikola Vlasic
WEST Ham wanaangalia pia uwezekano wa kumsajili winga wa CSKA Moscow na Croatia, Nikola Vlasic (23), kama mbadala wa kiungo mshambuliaji wa England, Jesse Lingard (28) kutoka Manchester United ambaye anatarajia kubakia Old Trafford. (Telegraph).

Neco Williams
MLINZI wa kulia wa Liverpool na Wales, Neco Williams huenda akasalia Anfield baada ya mbio za klabu zinavyomuwania kinda huyo mwenye miaka 20 kufifia katika wiki za karibuni. (Liverpool Echo).