Moussa Sissoko
KLABU ya Watford imeanza mazungumzo na Tottenham kuhusu uwezekano wa kumsajili kiungo Mfaransa Moussa Sissoko (32). (Fabrizio Romano).
Cristiano Ronaldo
MANCHESTER City na Juventus zimekubaliana kuhusu uhamisho wa mshambuliaji Mreno Cristiano Ronaldo (36), kujiunga na klabu hiyo.(AS).
Adama Traore
KLABU ya Wolverhampton Wanderers imekataa ofa ya mkopo kwa ajili ya winga wake raia wa Hispania, Adama Traore (25), kutoka Tottenham Hotspurs wakitaka kumbakisha. (Telegraph).
Nikola Vlasic
KLABU ya West Ham United inamnyemelea mshambuliaji wa CSKA Moscow na Croatia, Nikola Vlasic (23), wakiendelea kutafuta mbadala wa kiungo mshambuliaji wa Manchester United na England, Jesse Lingard. (Sky Sports).
Erling Braut Haaland
KLABU ya Paris St-Germain inaendelea kusaka wachezaji akiwemo kiungo wa Manchester United na Ufaransa, Paul Pogba (28), na mshambuliaji wa Borussia Dortmund na Norway Erling Braut Haaland (21), wakati huu wakijiandaa kumkosa Kylian Mbappe. (L’Equipe).
Kylian Mbappe
REAL Madrid imeongeza dau kufikia pauni milioni 145 kwa ajili ya mshambuliaji wa Ufaransa na PSG, Kylian Mbappe (22), baada ya dau lake la awali la pauni milioni 137 kukataliwa. (Sky Sports).
Noni Madueke
MANCHESTER United imemkosa winga wa timu ya taifa ya England chini ya miaka 21, Noni Madueke (19), baada ya nyota huyo kusaini mkataba mpya na klabu yake ya PSV Eindhoven. (Mirror).
Harry Kane
NAHODHA wa Tottenham na England, Harry Kane yuko kwenye mazungumzo kuhusu kuboresha mkataba wake. Mshambuliaji huyo mwenye umri wa miaka 28, anatarajia mshahara utakaofikia pauni 400,000 kwa wiki kupitia maboresho hayo baada ya kuamua kusalia klabuni hapo msimu huu. (Times).
Jules Kounde
CHELSEA wanakaribia kabisa kumsajili mlinzi wa Sevilla na Ufaransa, Jules Kounde (22), katika uhamisho utakaogharimu pauni milioni 42. (Sky Italia).
Kurt Zouma
WAKATI huo huo mlinzi wa kati wa Chelsea, Kurt Zouma (26), atafanyiwa vipimo vya afya kabla ya Mfaransa huyo kusaini mkataba wa miaka 5 na West Ham kwa uhamisho utakaogharimu pauni milioni 26. (Sun).
Weston McKennie
KLABU ya Tottenham imeanza mazungumzo kwa ajili ya kumsajili kiungo wa Juventus na Marekani, Weston McKennie (22) uhamisho utakaogharimu pauni milioni 40. (Independent).
Pierre-Emerick Aubameyang
MENEJA wa Arsenal, Mikel Arteta ametupilia mbali uwezekano wa nahodha na mshambuliaji wa Gabon, Pierre-Emerick Aubameyang kuondoka klabuni hapo. (ESPN).
Neal Maupay
KLABU ya Everton inamtaka mshambuliaji wa Brighton Mfaransa, Neal Maupay (25). (Sky Sports).
Declain Rice
MANCHESTER United inataka kusajili kiungo kabla ya dirisha la usajili kufungwa, lakini, itawapasa kusubiri kuona kama wanaweza kumpata kiungo wa England na West Ham, Declan Rice (22). (Independent).