RICHARLISON

PARIS ST-GERMAIN itajaribu kumsajili mshambuliaji wa Everton wa Brazil Richarlison, 24, ikiwa watakubali mpango wa kumuuza mshindi wa Kombe la Dunia la Ufaransa Kylian Mbappe, 22, kwa Real Madrid. (Sky Sports)

GABRIEL JESUS

PSG itamtaka mshambuliaji wa Manchester City wa Brazil Gabriel Jesus, 24, ikiwa Mbappe ataondoka. (Sun)

ERLING BRAUT HAALAND

MSHAMBULIAJI wa Borussia Dortmund wa Norway Erling Braut Haaland, 21, yupo kwenye rada za PSG endapo Mbappe ataondoka.(Star)

ODSONNE EDOUARD

EVERTON wamewasiliana na Celtic juu ya makubaliano ya mshambuliaji wa Ufaransa Odsonne Edouard, 23. (Sky Sports)

EDEN HAZARD

REAL MADRID wanamtaka winga wa Ubelgiji mwenye umri wa miaka 30, Eden Hazard, kiungo mshambuliaji wa Uhispania Marco Asensio, 25, au mshambuliaji wa Brazil Rodrygo, 20, wakati wanajiandaa kumtoa Mbappe. (Goal)

CRISTIANO RONALDO

JUVENTUS inamtaka Hazard kama mbadala wa mshambuliaji wa Ureno Cristiano Ronaldo, 36, ambaye amejiunga na Manchester United. (Marca)

EDINSON CAVANI

MSHAMBULIAJI wa Uruguay wa Manchester United Edinson Cavani, 34, “bado yuko katika mipango ya United msimu huu” na “hakuna mpango wa kumuuza” baada ya kuwasili kwa Ronaldo. (Goal)

ALEX FERGUSON

BOSI wa zamani wa United Sir Alex Ferguson alichukua jukumu kubwa kumshawishi  Ronaldo kurudi Old Trafford miaka 12 baada ya kuondoka kwenda Real Madrid. (Mirror)

SAUL NIGUEZ

CHELSEA imeshindwa kumsajili  kwa kiungo wa Atletico Madrid Saul Niguez baada ya mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 26 kutopewa uhakika wa kupata namba na bosi wa Blues Thomas Tuchel. (90 Min)

KURT ZOUMA

UHAMISHO wa Kurt Zouma wa Pauni milioni 25 kwenda West Ham kutoka Chelsea uko kwenye wasiwasi  baada ya shida na matibabu ya beki huyo wa Ufaransa mwenye umri wa miaka 26. (Mirror)

JULES KOUNDE

SEVILLA wanasema Chelsea wanaweza kukosa muda wa kumsajili beki wa Ufaransa Jules Kounde, 22, ambaye ana kifungu cha kutolewa cha pauni milioni 77.1. (FootballEspana)

ANDREAS CHRISTENSEN

CHELSEA wamekubali mkataba  mpya wa miaka minne na beki wa Denmark Andreas Christensen, na makubaliano ya mchezaji huyo wa miaka 25. (Goal)

AXEL WITSEL

ASTON VILLA wana nia ya kumsajili kiungo wa Ubelgiji Dortmund, Axel Witsel, 32. (Tuttosport – in Italian)