KYLIAN MBAPPE
REAL MADRID imejiondoa katika mazungumzo ya kumsajili mshambuliaji wa Ufaransa Kylian Mbappe, 22, kutoka Paris St-Germain kwasababu klabu haziwezi kukubali ada.(RMC Sport – in French)
EDUARDO CAMAVINGA
HATA hivyo, klabu hiyo ya Uhispania inatarajia kuipiku PSG katika mbio za kumsajili kiungo wa Ufaransa mwenye umri wa miaka 18 Eduardo Camavinga kutoka Rennes. (Canal+ via Get French Football News)
EDERSON
MANCHESTER CITY hawatarajii yeyote zaidi ama kuingia au kuondoka kabla ya dirisha la uhamisho kufungwa baada ya kumfungia kipa wa Brazil Ederson, 28, kwa mkataba mpya. Kiungo wa Ureno Bernardo Silva, 27, alikuwa ndiye gumzo katika ofa kutoka AC Milan, lakini hakufurahishwa na hatua hiyo. (Times – subscription required)
HECTOR BELLERIN
BARCELONA watajaribu kumsajili beki wa kulia wa Arsenal na Uhispania Hector Bellerin, 26, ikiwa mlinzi wa Brazil Emerson Royal, 22, ataondoka Nou Camp na kujiunga na Tottenham. (Mundo Deportivo – in Spanish)
NICOLAS TAGLIAFICO
WEST HAM wamefikia makubaliano ya maneno na Ajax kumsaini beki wa kushoto Nicolas Tagliafico, ingawa kukamilisha makubaliano hayo kabla ya tarehe ya mwisho uhamisho , Jumanne itakuwa vigumu na mchezaji huyo wa miaka 28 ambaye sasa hivi yuko katika jukumu la kimataifa na Argentina. (Telegraaf – in Dutch)
JULES KOUNDE
CHELSEA wamemuambia wakala wa beki wa kati wa Sevilla na Ufaransa Jules Kounde watafanya jaribio la mwisho kumsajili mchezaji huyo wa miaka 22. (ABC Sevilla, via Sport Witness)
CALLUM HUDSON-ODOI
LEICESTER CITY wameonyesha nia kwa winga wa Chelsea na England Callum Hudson-Odoi, 20, ambaye pia amehusishwa na Borussia Dortmund. (football.london)
TINO ANJORIN
KIUNGO wa kati wa Chelsea Tino Anjorin anakaribia kujiunga na Lokomotiv Moscow katika mkataba wa mkopo ambao unajumuisha chaguo la pauni milioni 17 kumnunua Mwingereza mwenye umri wa miaka 19. (Goal)