KAMPALA, UGANDA

DUKA  la Kitaifa la Tiba (NMS) limesema limeanza kupeleka katika vituo vya afya dawa za serikali zilizoagizwa .

Vituo vya afya hapo awali vilikuwa vikiagiza vifaa kutoka kwa NMS vikitumia fomu za mahitaji ya mkono katika ofisi za mkoa  au makao makuu huko Entebbe, ambayo ilikuwa na ufuatiliaji mbaya wa maagizo.

NMS ilisema katika taarifa yake kwamba vituo vya afya sasa vinaweza kuweka maagizo kwa kutumia jukwaa jipya la  lililoitwa NMS Plus, ambalo linalenga kuboresha ufanisi na uwazi.

“Utoaji wa kwanza wa dawa zilizoagizwa ulifanywa katika hospitali za rufaa za mkoa wa Moroto, Jinja, Mbale, Soroti,Kawolo, Buwenge, Kamuli, Masafu, Bududa, na hospitali kuu za Kayunga, pamoja na wilaya za Bududa na Manafwa.

Sheila Nduhukire, msemaji wa NMS, alisema vituo vya afya vinaweza kuweka maagizo yao mtandaoni ambapo NMS inapokea, inakataa au inakubali maagizo kulingana na bajeti ya hospitali.

Nduhukire alisema mchakato wa utafutaji wa habari, ambao unajumuisha ufuatiliaji wa wagonjwa wote wanaopokea dawa kutoka vituo vya afya, utakuwa muhimu katika kuondoa wizi wa dawa uliokithiri nchini.