NA SABRA MAKAME, SCCM
KAMANDA wa Polisi Mkoa huo, Kamishna Msaidizi wa Polisi ACP, Awadh Juma Haji, Watuhumiwa 11 waliokamatwa kwa tuhuma za kuiba nyaya za umeme kwenye taa za barabarani, bado hawajafikishwa Mahakamani kutokana uchunguzi wake kuendelea.
Akizungumzia na Zanzibar Leo juu ya tukio hilo lililotokea barabara ya Bububu na Mkapa Road hadi Mtoni, alisema wamelazimika kuwapa dhamana kutokana na ni haki yao kisheria na Polisi wanaendelea kufanya uchunguzi juu ya tuki hilo.
Awadh alisema baada ya kuwakamata watuhumiwa kumekua na muendelezo wa upelelezi katika maeneo mbali mbali kuhakikisha ushahidi unapatikana kwa watuhumiwa hao.
Aidha, alisema katika upelelezi huo wanahakikisha thamani halisi ya nyaya pamoja na taa zilizoathirika na wizi huo inapatikana .
“Ushahidi haujakamilika, endapo utapokamilika kesi Wataifikisha kwa Mkurugenzi wa Mashtaka na DPP atapojiridhisha ataweza kuandaa mashtaka na kuifikisha Mahakamani”alisema ACP Awadh.
Awadh alisema makosa ya wizi yanadhamana watuhumiwa wote wapo nje kutokana na dhamana ni haki ya kila mtu mpaka pale ushahidi utakapokamilika.
Watuhumiwa hao wanashikiliwa na Jeshi la Polisi, baada ya kukamatwa wakiwa na nyaya za umeme zilizoibiwa katika nguzo 175 ambazo kwa Wilaya ya Mjini zilikuwa 120 na Magharibi ‘A’ nguzo 55.
Hapo awali Jeshi la Polisi liliwakamata watu sita wakiwa katika eneo la tukio wakifanya wizi huo ambao walichangia kukamatwa watu wengine wanaodaiwa kuhusika na wizi huo wakiwemo watano wanaonunua bidhaa hiyo katika maduka ya chuma chakavu.