AMSTERDAM, Uholanzi
LOUIS van Gaal ameteuliwa kuwa kocha mkuu wa Uholanzi kwa mara ya tatu.
Mholanzi huyo mwenye umri wa miaka 69 anachukua nafasi ya Frank de Boer, ambaye alijiuzulu mwezi uliopita baada ya kushindwa kwenye hatua ya 16 bora na Jamhuri ya Czech kwenye Euro 2020.
Van Gaal alikuwa akikinoa kikosi hicho kutoka 2000-2002 na akareja tena 2012-2014 kabla ya kujiunga na Manchester United.
Hajafundisha tangu alipotemwa na United mnamo 2016 na akasema ilikuwa ‘heshima’ kurejea timu ya taifa ya Uholanzi.”Soka la Uholanzi limekuwa karibu na moyo wangu na kufundisha timu ya taifa ni nafasi muhimu ya kusogeza soka yetu mbele”, alisema, Van Gaal.(BBC Sports).