TEHRAN, IRAN

VIKOSI vinavyosaidiwa na Iran vinaaminiwa vimeiteka meli ya mafuta katika eneo la Ghuba nje ya pwani ya Umoja wa Falme za Kiarabu.

Hayo ni kwa mujibu wa duru tatu za usalama wa baharini baada ya wakala wa usalama wa baharini wa Uingereza kuripoti kuhusu uwezekano wa meli kutekwa katika eneo hilo.

Msemaji wa cheo cha juu wa jeshi la Iran amekanusha taarifa hizo akisema ni aina fulani ya vita vya kisaikolojia na ni njia ya kuandaa mazingira ya matukio mapya zaidi.

Meli hiyo iliyotekwa ilitambuliwa kama Asphalt Princess inayopeperusha bendera ya Panama katika eneo la bahari  ya Uarabuni kuelekea mlango wa bahari Hormuz.

Marekani ilisema ina wasiwasi na inachunguza ripoti za tukio hilo katika Ghuba ya Oman, lakini ni mapema kupitisha maamuzi.Uingereza ilisema inachunguza kwa haraka kisa hicho.