LONDON, England
WACHEZAJI wote wa klabu 20 za Ligi Kuu England wataendelea kupiga magoti kabla ya kuanza kwa michuano hiyo ikiwa ni ishara ya kupinga vitendo vinavyoashiria ubaguzi wa rangi.

Pamoja na hayo, katika jezi za wachezaji na maofisa kutakuwa na maandishi yanayopinga ubaguzi wa rangi ambapo mechi ya kwanza itachezwa kati ya wageni Brentford dhidi ya Arsenal, Ijumaa Agosti 13.

Awali, Brentford ilitangaza kuwa haitaendelea kupiga magoti kwa kile kilichoelezwa hakuna maana tena ya kupiga magoti.

Wachezaji walianza kupiga magoti Juni 2020 baada ya kukithiri kwa vitendo vya kibaguzi kwa wanamichezo kukiwa na kaulimbiu ya ‘Black Lives Matter’.

Mtendaji Mkuu wa EPL, Richard Masters, amesema, wachezaji, maofisa wataendelea kupiga magoti kuungana na wanamichezo wengine kupinga vitendo kama hivyo”.
Wachezaji watatu wa England walifanyiwa ubaguzi wa rangi baada ya kukosa penalti, Jadon Sancho, Bukayo Saka na Marcus Rashford kwenye michuano ya Euro 2020.(BBC Sports).