NA MWANAHAWA HARUNA SCCM
OFISA Uhusiano wa Wakala wa Chakula na Dawa Zanzibar, Zuwena Ngwali Makame, amewataka wafanyabiashara kuacha tabia ya kuingiza vyakula kwa kutumia bandari bubu, na badala yake kufuata utaratibu wa kupeleka kuchunguzwa, ili kuhakikisha jamii inatumia chakula salama.
Alisema hayo wakati akizungumza na Zanzibar Leo huko Ofisini kwake Mombasa Wilaya ya Magharib “B” Unguja, kuwa ni vizuri kwa wafanya biashara hao kufuata utaratibu wa kuchunguza Vinasaba vya Vyakula ili kuona vinafaa kwa matumizi ya binaadamu.
Pia amewataka wauzaji kuhifadhi vyakula hivyo sehemu salama baada ya kuhakikishwa vinafaa kwa matumizi ya binaadamu, ili viendelee kuwa salama kwa muda wote wa matumizi.
Aidha, aliwataka wafanya biashara kujali afya za watu na kuhakikisha kuwa wanauza chakula kilichokaguliwa na tayari kishafanyiwa uchunguzi na kuhakikishwa ni salama kwa binaadamu.
Zuwena amewataka badhii ya Wafanya biashara kuwacha tamaa kwa kukwepa kuhakikiwa chakula kwa kupitisha kimagendo au Bandari bubu na kuwataka wache kudha vyakula vilivyopitwa na wakati.
“Wafanya biashara wazijali Afya na wananchi waache tamaa na wapitishe chakula sehemu salama ambazo zimethibitishwa ikiwemo bandari halali kwani tunawakaguzi wetu wanafanya kazi sehemu hizo na wache kutumia bandari bubu kitu ambacho kinahatarisha Afya za watu.
Vilevile, ameitaka jamii kushirikiana na tasisi hiyo kwa kutoa tarifa juu ya Wafanya biashara ambao wanaenda kinyume na sheria na watahakikisha usalama kwa kuwahifadhi watoaji wa taarifa hizo.
Nae, Sabrina Haji muzaji wa duka la vyakula amewataka Wafanya biashara wenzake kuwacha tabia ya kuuza vyakula vilivyo pitwa na wakati kwa kuepusha gharama na kuwataka waweze kujali Afya za wateja wao.