MOGADISHU, SOMALIA

WATU wawili wameuwawa na wengine wamejeruhiwa katika shambulizi la bomu mjini Mogadishu, Somalia.

Kwa mujibu wa polisi na watu walioshuhudia, mshambuliaji wa kujitoa muhanga aliripua bomu ndani ya mgahawa wa chai  karibu na eneo la njia panda lililokuwa na watu wengi kaskazini mwa Mogadishu.

Ofisa wa polisi wa trafiki Mohammed Ali ambaye alikuwa katika eneo la tukio, alisema shambulizi hilo liliwaua maofisa wawili wa usalama na kuwajeruhi watu wengine watano.

Inaripotiwa maofisa wengi wa usalama wa vikosi vya Somalia na raia hulitembelea eneo hilo.

Kwa mujibu wa shirika la ujasusi lisilo la kiserikali la Marekani linalofuatilia mienendo ya makundi ya kigaidi na yenye misimamo mikali, SITE, kundi la Al Shabaab lenye mahusiano na mtandao wa kigaidi wa Al-Qaeda limedai kuhusika na hujuma hiyo.