KIGALI, RWANDA

WAWEKEZAJI wa Rwanda wamehimizwa kutumia fursa zinazotolewa na mpango mpya uliosainiwa kati ya Shirikisho la Sekta Binafsi na Mfuko wa Mshikamano wa Afrika ili kuhakikisha upatikanaji zaidi wa mikopo ya uwekezaji.

Wito huo ulitolewa wakati wa hafla ya utiaji saini iliyofanyika kati ya mwenyekiti wa PSF, Robert Bafakulera na Ahmadou Abdoulaye Diallo, mkurugenzi mkuu wa Mfuko wa Mshikamano wa Afrika.

Kwa hisani ya ushirikiano huu, biashara za Rwanda zina uwezo wa kupata mikopo kupitia vituo vya mkopo vinavyoungwa mkono na ASF kwa miradi ya uwekezaji iliyofikia 80%.

Pia wafanyabiashara wanaweza kuomba kufadhiliwa tena na  mfuko wa usimamizi wa mtu mwengine ili kufufua biashara zao.

Bafakulera alisema kuwa hiyo ni fursa nzuri kwa jamii ya wafanyabiashara wa Rwanda.

“Ushirikiano huu unamaanisha mengi kwa sekta binafsi, haswa wale walioathiriwa na Covid-19, ambayo wakati mwengine ilifanya iwe ngumu kwao kulipa mkopo au kupata mitaji ya kuanzisha biashara,”alisema.

Athari za Covid-19 na hasara zilizotokana na mazingira tofauti zilikuwa vizuizi vikuu vya biashara kustawi katika nchi nyingi za Kiafrika.

Kwa upande wake, Diallo alisifu urahisi wa Rwanda wa kufanya biashara na kuelezea kuwa taasisi yake inataka kuongeza hatua za kibiashara na Rwanda ambayo ndiyo sababu ya kuchagua  kutia saini na nchi hiyo.

Baada ya kusikiliza mawasilisho ya kile ASF inafanya, Teddy Ndayambaje, mwekezaji ambaye aliwakilisha kampuni ya utengenezaji wa chuma wa eneo hilo alisema kampuni yake ilikuwa tayari kushirikiana na mfuko huo akisema kwamba iliongeza njia kwa dhamana ya ufadhili ambayo ilikuwa moja ya changamoto za kuvunja ardhi zinazokabiliwa na jamii ya wafanyabiashara wa Rwanda.