NA TIMA SALEHE, DAR ES SALAAM

ALIYEKUWA mshambuliaji wa kikosi cha Yanga SC, Waziri Junior amewaaga mashabiki wake wa klabu hiyo.Waziri alisajiliwa na Yanga msimu uliopita akitokea Mbao FC ya mkoani Mwanza, ambayo ilishuka daraja.

Waziri ni miongoni mwa washambuliaji ambao wamezitumikia klabu mbalimbali kwenye ligi kuu Tanzania Bara kama ikiwemo Azam FC.

Akizungumza na Zanzibar Leo  juu ya kuondoka kwake Yanga, alisema ameachana na mabosi wake hao kwa sababu sio sehemu ya mpango wao kwa msimu ujao.

Alisema alikuwa hajamaliza mkataba wake lakini walikaachini nakuangalia ni namna gani anaweza kuondoka bila kutolewa kwa mkopo.

“Vipo klabu tofauti tofauti vya ndani ambavyo zimeonyesha kunihitaji siwezi kuvitaja kwa sasa lakini muda utakapofika mtaona wapo nimeenda,”alisemaAlisema yeye ni mchezaji na maisha yake yanategemea mpira hivyo anaangalia timu yenye ofa nzuri kwake ataenda huko.