NA MWAJUMA JUMA

HARAKATI za kuwania shilingi milioni 10 za michuano ya yamle yamle zinazidi kuendelea kwa kasi baada ya juzi timu ya Jambiani 4G kuifunga Malaysia bao 1-0.

Mchezo huo ambao umewarahisishia Jambiani kusonga mbele katika michuano hiyo, ulichezwa uwanja wa Amaan nje majira ya saa 10:00 za jioni.

Katika mchezo huo Jambiani ambayo ilikuwa na kila sababu ya kutaka kushinda bao lake hilo la pekee liliwekwa kimiyani na mchezaji Othman Makame.

Aidha katika uwanja wa Magirisi kulikuwa na mchezo kati ya Mapembe City na Anfield ambao ulimalizika kwa wanaume hao kutoka sare ya kutokufungana.