NA TIMA SALEHE, DAR ES SALAAM

KLABU ya Yanga imekamilisha usajili wa mchezaji wa kimataifa kutoka nchini Uganda Khalid Aucho.

Kabla ya kutua Yanga Aucho alikuwa anakitumikia kikosi cha Lel Makasaa inayoshiriki ligi kuu ya Misri.

Mchezaji huyo ametambulishwa jana kwenye ukurasa wa kijamii wa ‘Instagram’ wa klabu hiyo.

Katika utambulisho wake wa video mchezaji huyo amesema yeye sasa ni wanjano na kijani akimaanisha Yanga.

Alisema mchezaji mkubwa kwenye timu kubwa yenye ndoto kubwa. Aucho pia ni mchezaji wa timu ya taifa ya Uganda Cranes.

Wakati huo huo taarifa rasmi kutoka kwenye klabu hiyo zimeeleza kwamba klabu hiyo, imeachana rasmi na mchezaji wake mzawa kipa Metacha Mnata.