NA TIMA SALEHE, DAR ES SALAAM

MCHEZO wa Ngao ya Hisani unatarajiwa kuchezwa Septemba 25 Mwaka huu.Mchezo huo utawakutanisha mabingwa wa ligi kuu Tanzania Bara Simba na mshindi wa pili wa michuano hiyo Yanga ambao ni watani zao wa jadi.

Mechi hiyo itachezwa kwenye Uwanja wa Benjamini Mkapa jijini Dar es Salaam, kwa lengo la kufungua rasmi msimu wa mashindano 2021/2022.

Taarifa hiyo ilitumwa kwenye ukurasa wa mtandao wa kijamii wa Shirikisho la Soka la Tanzania.

Ikumbukwe bingwa mtetezi wa michuano hiyo ni Simba SC ambao pia ni  mabingwa wa ligi kuu ya Tanzania na Kombe la Shirikisho la Azam kwa msimu uliopita.