NA MWANAJUMA MMANGA
WAJUMBE wa Kamati ya Kilimo, Biashara na Utalii ya Baraza la Wawakilishi imeshauri Taasisi ya Viwango Zanzibar (ZBS) kuongeza kasi katika ukaguzi wa bidhaa hasa zinazotoka nje ili kuepuka nchi kuwa jaa la kutupia bidhaa.
Mwenyekiti wa kamati hiyo Yussuf Hassan Iddi aliyasema hayo wakati walipofanya ziara ya kutembelea taasisi hiyo huko Amani mjini Unguja.
Alisema kutokufanya hivyo kunaweza kuathiri hali ya biashara hasa ukizingatia kuwa dunia imeelekea zaidi katika ushindani wa kibiashara.
Alisema kumekuwa na ubababishaji katika uingizaji wa bidhaa unaofanywa na wafanyabiashara wasiokuwa waaminifu wakiwa na lengo la kujipatia fedha pasipo kujali afya za watumishi hivyo umakini wao utafanya nchi kuwa salama dhidi ya bidhaa hizo.
“Zinapoingia bidhaa ambazo hazina ubora na ni mbovu zinaathii sana na kusabaisha athari za mlaji ukizingatia hasa zile za makopo, na zile zilizofungashiwa sambamba na zile za majimaji hupelekea maradhi ya kensa,” alisema Menyekiti huyo.
Hivyo aliiomba ZBS kuhakikisha wanafatilia maeneo yanayopitshwa bidhaa hizo ikiwemo bandarini, viwanja vya ndege pamoja maeneo ya kuhifadhia vyakula ama bidhaa katika maghala ili kulinda usalama ya mlaji.
Aidha walishauri umuhimu wa kuimarisha ofisi za taasisi ya zbs katika kisiwa cha Pemba ili kuweza kufanya kazi zake ikiwemo upimaji bidhaa zinazotengenezwa na wajasiri amali wa kisiwa hicho badala ya kulazimika kuleta unguja.