NA ABDI SULEIMAN

TIMU ya Shirika la Umeme (ZECO) Tawi la Pemba, imeshindwa kutetea ubingwa wake wa mashindano ya Mawizara Pemba, baada ya kutandikwa mabao 2-0 na Wizara ya Afya.

Mchezo huo wa nusu fainali ya pili ulipigwa katika uwanja wa Gombani huku ukishuhudiwa na mashabiki wengi wa soka, kutokana na ushindani wa timu hizo katika mashindano hayo.

katika mtanange huo mchezaji Mohamed Salim aliipatia timu yake ya Afya balo la kuongoza dakika ya 17, huku ZECO ikijitahidi kusawazisha lakini jitihada zao zimegonga wa mwamba uwanjani hapo na kwenda mapumziko bao 1-0.

Kipindi cha pili kilianza kwa kasi kubwa huku kila timu ikirudi kwa matumaini mapya, Afya kuongeza bao na ZECO kurudisha.

Dakika 67 Suleiman Ismail aliipatia bao la pili nakufuta matumaini ya timu ya ZECO.

Kwa matokeo hayo timu ya Utalii itakutana na Afya kwenye mchezo wa fainali utakapigwa kesho katika uwanja wa Gombani, huku Mawasiliano na ZECO watakutana kutafuta mshindi wa tatu.