NA MWAJUMA JUMA

WAFANYAKAZI wa timu ya soka ya Bodi ya Mapato Zanzibar (ZRB) juzi walishindwa kutamba mbele ya waandishi wa Habari kwa kuruhusu kufungwa mabao 3-2 katika mchezo wa kirafiki uliochezwa Mao Zedong B.

Mchezo huo ulichezwa majira ya saa 1:00 usiku na kuonekana kuwa na ushindani kiasi.

Katika mchezo huo timu ya Waandishi wa Habari za Michezo (ZASWA), ilionesha dalili za ushindi na mapema kutokana na kuwazidi kwa kila idara wapinzani wao hao.

Wakicheza kwa kusomana na tabia miamba hiyo hadi mapumziko ZASWA walikuwa wakiongoza kwa kwa mabao 3-0, ambayo yalifungwa na Is-haka Manti, Abubakar Harith na Kheri Abdukadir.

Kwa upande wa timu ya ZRB mabao yao yalifungwa na  Lukman Kassim na Muumini Ali Suleiman.