NA KHAMISUU ABDALLAH

WANANCHI wa Zanzibar wameombwa kujitokeza kwa wingi katika tamasha la muziki linalotarajiwa kufanyika Agosti 21 mwaka huu katika viwanja vya Amaan.

Akizungumza na vyombo vya habari ofisini kwake Kikwajuni kuhusu tamasha hilo,Waziri wa Utalii na Mambo ya Kale, Lela Mohammed Mussa.

Alisema tamasha hilo lililoandaliwa na msanii wa muziki wa bongo fleva Zuhura Othman Sudi maarufu Zuchu, lina lengo la kuinua vipaji vya wasanii wachanga wa Zanzibar katika muziki.

Alisema ikiwa wananchi watamuunga mkono mzanzibari mwenzao basi kwa kiasi kikubwa italeta hamasa kwa msanii huyo kuona lengo alilokusudiwa linafikiwa.

Aliwatoa hofu wananchi na kusema kuwa siku hiyo maeneo yote ya viwanja hivyo, kutakuwa ba usalama wa kutosha kupitia vyombo vya ulinzi na usalama vya serikali.

Aidha alisema  msanii Zuchu ambae pia ni balozi wa utalii wa Zanzibar amefanya tamasha hilo kwa lengo la kuinua vipaji vya wasanii wachanga wa Zanzibar.

Hata hivyo alisena tamasha hilo litajumuisha

sanaa mbalimbali ikiwemo taarabu, bongo fleva na ngoma nyengine za asili.

Alisema jumla ya wanamuziki 20 watatumbuiza katika tamasha wakiwemo kutoka Tanzania bara na Zanzibar