BARCELONA, Hispania
MAUMIVU aliyoyapata Sergio Aguero yanaifanya Barcelona kuikosa huduma yake, lakini, ameanza mazoezi madogo madogo tokea aanze kupata nafuu ya maumivu ya nyama za mguu.

Aguero ambaye alijiunga na Barcelona akitokea Manchester City kwenye usajili wa bure majira ya kiangazi, na mpaka sasa bado hajacheza mechi hata moja tokea ajiunge na miamba hao wenye makazi yao jiji Barcelona.

Barcelona inatarajia kupata huduma ya Aguero kuanzia kati kati ya mwezi wa 10 japo inamuhitaji wakati huu kwani imepoteza wachezaji wake hatari kama Lionel Messi ambaye amesajiliwa na Paris Saint Germain huku Antonio Griezman akirejea Atletico de Madrid kwa mkopo.

Aguero amesini dili la miaka miwili na miamba hiyo huku kukiwa na matarajio makubwa kwa klabu, kwani alionyesha makali yake akiwa na Manchester City ambapo aliifungia magoli 184 katika michezo 277.Aguero mwenye umri wa miaka 33 anatarajiwa kuendeleza makali yake ya akiwa na Barcelona japo anapitia kipindi cha maumivu ya mara kwa mara. (Goal).