MADRID, Hispania
BEKI, David Alaba, amefichua siri ya kuwa hakuitaka jezi namba nne ambayo awali ilikuwa inavaliwa na mkongwe Sergio Ramos ambaye amehamia Paris Saint Germain.

Ramos ambaye ameivaa jezi hiyo kwa miaka yake 16 aliyokuwepo Real Madrid huku akiwa ameshinda makombe matano ya La Liga na Mabingwa Ulaya manne.

Mchezaji huyo wa Austria alitaka apatiwe nambari ya jezi ambayo alikuwa akiivaa kwa zaidi ya miaka 10 akiwa na miamba ya Ujerumani ya Bayern namba 27 kwa sababu hakutaka kufananishwa na mchezaji yeyote.

Jezi nambari 27 aliyokuwa anaitaka Alaba, hairuhusiwi kuvaliwa na yeyote ambaye hakutokea kwenye akademia ndani ya La Liga na klabu ikamchagulia nambari 4. (Goal).